KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Saturday, December 4, 2010

Opoku Agyemang AIPA 5 QATAR.


Pongezi kwa nchi ya Qatar iliyofanikiwa kupata nafasi ya kuwa mwenyeji wa fainali za kombe la dunia za mwaka 2022 zimeendelea kutolewa kutoka kwa wadau mbali mbali wa mchezo wa soka ulimwenguni kote.

Moja ya pongezi hizo zimetolewa na winga wa kimataifa toka nchini Ghana pamoja na klabu ya Al-Ahly Doha Sports ya nchini Qatar Opoku Agyemang ambapo amesema nchi hiyo ina vigezo vinavyokidhi haja ya kuandaa fainali hizo ambazo zitachezwa kwa mara ya kwanza katika ukanda wa mashariki ya kati.

Amesema toka apoanza kucheza soka nchini humo mwaka 2009 amekua ajifunza mambo mengi yanayohusiana na soka ambapo kwa upande wake ameona yanafaa katika harakati za nchi hiyo kupata nafasi hiyo muhimu ambayo pia ilikua ikiwaniwa na mataifa mbali mbali yenye nguvu dunuani.

Hata hivyo winga huyo mwenye umri wa miaka 21 amebainisha kwamba anatambua yapo mataifa mengine yamechukizwa na nchi ya Qatar kutangazwa mshindi katika kinyng’anyiro cha kuwa mwenyeji wa fainali za kombe la dunia za mwaka 2022 lakini akazitaka nchi hizo kuelewa kwamba nchi ya Qatar hakuna inachoshindwa kufanya katika soka kama ilivyo kwenye nchi nyingine duniani zilizowahi kuandaa fainali kubwa za soka duniani.

Nchi ya Qatar iliibuka kidedea baada ya kuzibwaga nchi za Australia; Japan; Marekani na Korea Kusini.

No comments:

Post a Comment