
Uongozi wa klabu ya Ajax Amsterdam umethibitisha taarifa za kuondoka kwa meneja Martin Jol ambae ameamua kujiuzulu kwa utashi wake binafsi.
Uongozi wa klabu hiyo umethibitisha suala hilo kupitia taarifa zilizochapishwa kwenye mtandao wa klabu ambapo umetoa shukurani za dhati kwa meneja huyo ambae kwa asilimia kubwa alionyesha malengo mazuri ya kutimiza malengo ya Ajax Amsterdam msimu huu.
Marton Jol amesema ameondoka Amsterdam Arena huku akiwa bado anapapenda kwa moyo wake wa dhati lakini kilichomfanya kufikia maamuzi hayo ni uongozi wa ngazi za juu kushindwa kumtimizia aliyokua akiyahitaji kwa malengo ya kufikia mikakati iliyowekwa.
Jol ameondoka klabuni hapo huku akikiacha kikosi cha klabu ya Ajax Amsterdam kikiwa katika nafasi ya nne kwenye msimamo wa ligi kuu ya nchini Uholanzi huku kikiwadai vinara wa ligi hiyo PSV Eindhoven point.
Tayari uongozi wa klabu ya Ajax umetangaza kumchukua kocha msaidizi wa timu ya taifa ya Uholanzi Frank de Boer kwa mkataba wa miezi sita huku kibarua chake cha kwanza kikitarajiwa kuwa kesho kwenye mchezo wa ligi ya mabingwa barani Ulaya dhidi ya Ac Milan.
Wakati huo huo Marton Jol mwenye umri wa miaka 54 tayari ameshaanza kuhusishwa na taarifa za kutaka kuchukuliwa na uongozi wa klabu ya Newcastle United, kwa lengo la kuziba nafasi iliyoachwa wazi na Chris Hughton alietimuliwa kazi jana jioni.
No comments:
Post a Comment