KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Thursday, December 30, 2010

KILA MMOJA ANA NAFASI YA KUCHEZA !!


Kamanda wa jeshi la Ashburton Grove Arsene Wenger ametetea maamuzi ya kushusha kikosi tofauti kwenye mchezo wa jana walipocheza na wenyeji wao Wigan Atheletic.

Wenger amesema ilimlazimu kufanya hivyo kutokana na kuwaamini vilivyo wachezaji wake ambao wamekua wakifanya vyema hivyo haoni sababu ya mashabiki kuhoji kwa nini alifanya maamuzi hayo ya kuwatumia wachezaji wanane tofauti ambao hawakucheza mchezo uliopita dhidi ya Chelsea.

Arsene wenger mwenye umri wa miaka 61 amesema hana budi kufanya maamuzi hayo kwa lengo la kutao nafasi kwa wachezaji wake kupumzika hasa ikizingatiwa katika kipindi hiki cha kuelekea sikuku ya mwaka mpya kumekua na michezo mingi ambayo hawezi kutumia kikosi kimoja kila panapokucha.

Akizungumzia mazingira ay mchezo wa jana Wenger amesema walikua na sababu ya kuibuka na ushindi kufuatia wachezaji wake kuonyesha uwezo mkubwa lakini mwishoni mwa mchezo huo walijikuta wakipata point moja licha ya kuongoza kwa muda mrefu mabao mawili kwa moja.

Wakati huo huo nahodha na kiungo wa klabu ya Arsenal Cesc Fabregas amemlaumu muamuzi wa mchezo wa jana Lee Probert kwa kushindwa kutoa maamuzi sahihi ya kuipa penati timu yake katika dakika za mwisho baada ya James McArthur kuunawa mpira wa adhabu uliopigwa na kiungo wa kimataifa toka nchini Ufaransa Samir Nasri.

Amesema muamuzi huyo alistahili kuwa na maamuzi sahihi kufuatia kosa lililofanywa na mchezaji huyo kuonekana dhahiri lakini cha kushangaza hafanya chochote zaidi ya kuonyesha iashara ya kukataa.

Cesc Fabregas amemtupio lawama muamuzi huyo wa kiingereza huku akikumbushia kosa kama hilo, lilivyomtokea yeye kwenye mchezo dhidi ya Tottenham Hotspurs ambao walipata bao la kusawazisha kwa mkwaju wa penati baada ya yeye kuunawa mpira katika eneo la hatari kama ilivyokuwa kwenye mchezo wa jana.

No comments:

Post a Comment