

Baada ya aliekua meneja wa klabu ya Newcastle Utd Chris Hughton kutimulia kazi jana jioni, tayari fununu zimeshaanza kuibuka huku ikidaiwa kuwa huenda nafasi ya meneja huyo wa kiingereza ikajazwa na Martin O’Neil aliekua akikinoa kikosi cha Aston Villa msimu uliopita pamoja na Martin jol ambae ametangaza kujiuzulu kukifundisha kikosi cha Ajax Amsterdam ya nchini Uholanzi.
Mameneja hao wawili wamekua wakitajwa sana na vyombo vya habari sambamba na mashabiki wa klabu ya Newcastle Utd ambao mapema hii leo kila mmoja alisikika akimsikia mmoja wa mameneja hao wawili.
Taarifa zilizotolewa hii leo asubuhi kupitia vyombo mbali mbali vya habari, zilieleza kwamba Maratin Jol alikua na nafasi kubwa sana ya kutangazwa kuwa meneja wa klabu ya Newcastle Utd lakini muda ulivyozidi kusogea jina la Martin O’Neil nalo likatajwa hatua ambayo iliwafanya mashabiki wa The Magpies kuzungumza huku na kule.
Miongoni wa mashabiki hao wamesema kwa kiasi kikubwa mameneja hao wote wana uwezo mkubwa wa kukiongoza kikosi cha Newcastle Utd na kikafanikiwa kufikia malengo yaliyowekwa hivyo wanaona maamuzi yaliyochukuliwa na viongozi wao ya kuwaweka kwenye kinya’nyiro cha kuwani nafasi ya Hughton ni sahihi.
Hata hivyo mashabiki wengine wa klabu hiyo bado waliendelea na msimamo wa kumsifia meneja ambae wanaona anafaa kati ya hao wawili.
Wakati huo huo chama cha mameneja wa vilabu nchini uingereza kimeelezea masikitiko yake ya kutimuliwa kazi kwa Chris Hughton alieirejeshea heshima Newcastle Utd baada ya kuiwezesha kucheza ligi kuu ya soka nchini humo kwa mara nyingine tena kufuatia dhoruba la kushuka daraja misimu miwili iliyopita.
Mtendaji mkuu wa chama hicho Richard Bevan amesema taarifa za kutimuliwa kazi za Hughton zilipotolewa jana jioni ziliwashtua na kufikia hatua ya kujiuliza maswali nini chanzo cha kutimuliwa kwake ili hali alikua akiendelea kufanya vyema katika shughuli zake za kukiongoza kikosi cha The Magpies.
Amesema meneja huyo msimu uliopita alijitahidi kwa uwezo wake wote kwa kuiwezesh Newcastle Utd kucheza kwa hali na mali na kufanikiwa kujikusanyia point 102 ambazo ziliirejesha klabu hiyo kwenye ligi kuu huku akiweka rekodi ya kipee ya kucheza michezo 17 pasipo kufungwa mchezo hata mmoja wa ligi daraja la kwanza.
Kwa upande wake Chris Hughton amesema hana budi kukujishukuru yeye binafsi kwa kazi nzuri aliyoifanya ndani ya klabu hiyo na ana imani kubwa mchango wake utaendelea kukumbukwa na kuheshimiwa pia.
Kutimuliwa kazi kwa meneja huyo kumekuja siku moja baada ya kikosi cha Newcastle Utd kutembezewa kichapo cha mabao matatu kwa moja na West Brom Albion.
No comments:
Post a Comment