
Ndoto za klabu ya Arsenal ya kutaka kumsajili kipa wa kimataifa toka nchini Australia pamoja na klabu ya Fulham Mark Schwarzer zimefutika kufuatia kipa huyo kukubalia kusaini mkataba mpya na The Cottagers.
Mark Schwarzer mwenye umri wa miaka 38 amekubali kusaini mkataba mpya na klabu hiyo inayomilikiwa na taykun wa kiarabu toka nchini Misri Mohamed Abdel Moneim Al-Fayed ambao utamuweka klabuni hapo hadi mwaka 2012.
Meneja wa klabu ya Fulham Mark Hughes ameonyesha kufurahishwa na kitendo cha kuendelea kuwa na kipa huyo ambapo amesema anaamini sasa kikosi chake kilichojaa damu change kitaendelea kukomazwa na ushauri Mark Schwarzer ambae mara nyingi huchukua muda wake kuwashauri wachezaji wenzake.
Nae Mark Schwarzer akatoboa siri iliyomfanya akubalai kusaini mkataba huo kwa kusema kwamba mahusiano mazuri yaliopo kati yake ya Mark Hughes yamekua chachu ya kufikia hapo alipo hivyo aliona hana budi kukubalia kubaki Croven Cottage.
Mark Schwarzer alisajiliwa na klabu ya Fulham mwaka 2008 akitokea klabu ya Middlesbrough kwa uhamisho huru.
No comments:
Post a Comment