KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Monday, December 6, 2010

TUZO YA DUNIA KWENDA BARCELONA.



Wachezaji watatu wa klabu bingwa nchini Hispania FC Barcelona Xavi Harnandes, Andres Iniesta pamoja na Lionel Messi wamesalia kwenye kinyang’anyiro cha kuwania tuzo ya mchezaji bora wa dunia ambayo hutolewa kila msimu na shirikisho la soka ulimwenguni FIFA.

Wachezaji hao watatu wamesalia katika kinyang’anyiro hicho baada ya kufanyika kwa mchujo wa wachezaji waliotajwa kwenye orodha ya kuwania tuzo hiyo ambapo kwa mara ya kwanza orodha ilikua na jumla ya wachezaji 23.

Licha ya kusalia wachezji watatu wanaocheza kwenye klabu moja tayari kuna baadhi ya wadadisi wa soka barani Ulaya wameshaanza kuhusi huenda kiungo wa kimataifa toka nchini Argentina Lionel Messi akatwaa kwa mara nyingine tena tuzo hiyo baada ya kufanya hivyo msimu uliopita.

Kigezo kikubwa kinachotajwa huenda kikamuwezesha kiungo huyo mwenye umri wa miaka 23 kutwaa kwa mara nyingine tuzo ya uchezaji bora duniani ni kufuatia uwezo wake mkubwa anaouonyesha akiwa na klabu yake ya Barcelona ambayo msimu huu inatetea taji la nchini Hispania kwa mara ya pili mfululizo.

Xavi Harnades pamoja na Adres Iniesta wote kwa pamoja wanabebwa na sifa ya kuiwezesha nchi ya Hispania kutwaa ubingwa wa dunia mwaka huu 2010 lakini bado wanaonekana kutomfikia Messi ambae kwa asilimia kubwa anatajwa sana na wadadisi wa soka katika kinyang’anyiro hicho.

Kwa upande wa tuzo ya kocha bora wa mwaka kocha mkuu wa timu ya taifa ya Hispania Vicente del Bosque, meneja wa klabu ya Barcelona Pep Guardiola pamoja na meneja wa klabu ya Real Madrid Jose Mourinho wametajwa kuwania tuzo hiyo ya msimu wa mwaka 2010-11.

Hafla ya kuwatangaza washindi wa tuzo hizo bora za dunia zinatarajia kufanyika mjini Zurich nchini Uswiz Januari 10 mwaka 2011.

No comments:

Post a Comment