Mshambuliaji wa kimataifa toka nchini Togo Emmanuel Sheyi Adebayor amesema bado ana matumaini ya kurejea tena katika klabu ya Man City iliyomtoa kwa mkopo na kumpelekea huko Estadio Stantiago Benabeu nchini Hispania.
Emmanuel Sheyi Adebayor ambae tayari ameshakamilisha mipango ya kuichezea Real Madrid kwa mkopo ametoa msimamo huo saa chache baada ya kukabidhiswa jezi ya klabu hiyo na mkurugenzi wa michezo Jorge valdano.
Amesema binafsi bado anaipenda klabu ya Man City na bado ataendelea kuipenda hivyo halitokua jambo la ajabu kwake uongozi wa klabu hiyo ukaonyesha matumaini ya kumuhitaji kwa mara nyingine tena kurejea huko City Of Manchester aliposajiliwa akitokea Arsenal ya jijini London.
Amesema kwake bado ana iona nafasi ya kuitumikia klabu hiyo ndani ya kikosi cha Mancini ambacho kwa sasa kimesheheni washambuliaji kama Super Mario Balotelli, Edin Dzeko pamoja na Carlos Tevez.
Hata hivyo licha ya kuzungumza maneno hayo Emmanuel Sheyi Adebayor bado ana haki ya kurejea katika klabu hiyo mwishoni mwa msimu huu baada ya mkataba wake wa kuitumikia klabu ya Real Madrid kufikia kikomo.
Endapo uongozi wa Peal Madrid utahitaji asalie huko mjini Madrid utalazimika kulipa kiasi cha paund million 16 kama ada ya uhamisho wa mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 26.
No comments:
Post a Comment