KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Thursday, January 27, 2011

GRANT AKIRI UDHAIFU WA KIKOSI CHAKE.


Baada ya kutupwa nje katika michuano ya kombe la ligi * Curling Cup* ambayo sasa imeingia katika hatua ya fainali, meneja wa klabu ya west ham Utd Avram Grant amesema makosa ya ulinzi yaliyofanywa na wachezaji wake katika mchezo wa kuamkia hii leo dhidi ya Birmingham City, yaliwagharimu kwa kiasi kikubwa.

Grant aliekua na matumaini makubwa ya kutinga katika hatua ya fainali kufuatia ushindi wa mabao mawili kwa moja alioupata Januari 11 huko Upton Park, amesema kiujumla kikosi chake kilionyesha soka safi ndani ya 45 za kipindi cha kwanza lakini udhaifu wa ulinzi ulianza kujitikeza katika dakika 45 za kipindi cha pili.

Amesema kupata bao la kuongoza lililofungwa na mshambuliaji wake wa kimataifa toka nchini Uingereza Carlton Michael Cole Okirie kuliongeza ari ya kujituma kwa wachezaji wake hadi kipindi cha kwanza kilipomalizika lakini cha kushangaza hakukuwa na juhudi za kuhakikisha bao hilo linadumu hadi mwishoni mwa mpambano huo ambao ulilazimika kuchezwa ndani ya dakika 120 kufuatia timu hizo kwenda sare ya mabao matatu kwa matatu kiujumla.

Kwa upande wake meneja wa klabu ya Birmingham City Alex McLeish amesema kutulia na kujituma kwa wachezaji wake kulimfanya atulize akili na kutoa mchango kidogo wa mawazo pale kikosi chake kiliporejea katika chumba cha kubadilishia wakati wa mapumziko huku kikiwa nyuma kwa idadi ya bao moja kwa sifuri.

Amesema baada ya wachezaji wake kurejea uwanjani walifanya kazi iliyotakikana na kudhihirisha uwezo wao ambao umemfurahisha kila mmoja huko St Andrews pamoja na shabiki yoyote anaeishabikiwa Birmingham City popote ulimwenguni.

Kwa matokeo hayo sasa Birmingham City watakutana uso kwa uso na jeshi la Ashburton Grove Arsenal katika mchezo wa hatua ya fainali ya michuano hiyo ya kombe la ligi *Curling CUP* Februari 27 kwenye uwanja wa Wembley uliopo jijini London.

No comments:

Post a Comment