Uongozi wa klabu ya Liverpool umeiweka kapuni ofa ya klabu bingwa nchini Uingereza Chelsea iliyokua inamlenga mshambuliaji wa kimataifa toka nchini Hispania Fernando José Torres Sanz.
Msemaji wa klabu ya Liverpool amethibitisha kuwekwa kapuni kwa ofa hiyo ambapo amesema uongozi wa ngazi za juu wala haukuhitaji kujadili suala hilo kwa sababu halina nafasi ya kuzungumza katika kipindi hiki.
Amesema ofa hiyo iliyotumwa kutoka Stamford Bridge imeonyesha kuwa Chelsea wapo tayari kutoa kiasi cha paund million 40 kama ada ya uhamisho wa mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 26.
Msemaji huyo ameendelea kueleza kwamba Fernando José Torres Sanz ambae ni miongoni mwa wachezaji walioiwezesha timu ya taifa ya Hispania kutwaa ubingwa wa dunia mwaka 2010 huko nchini Afrika kusini, kwa sasa anahangaikia suala la kurejea katika kiwango chake cha kawaida baada ya kuuanza ovyo msimu huu chini ya meneja aliefungasha virago Roy Hodgson.
Hata hivyo tayari meneja wa klabu ya Liverpool Kenny Dalglish ameshaeleza wazi kwamba hategemei kukibomoa kikosi chake cha kwanza kwa kuwauza wachezaji muhimu kufuatia kuwa katika harakati za kuirejeshea heshima Liverpool.
Kama itakumbukwa vyema Fernando José Torres Sanz, alisajiliwa na Liverpool mwaka 2007 akitokea nchini kwao Hispania kwenye klabu ya Atletico Madrid kwa ada ya uhamisho wa paund million 20.
kipindi hiki.
No comments:
Post a Comment