KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Friday, January 28, 2011

ADEBAYOR NA MANCINI WANAIVA?


Baada ya mshambulaiji wa kimayaifa toka nchini Togo Emmanuel Sheyi Adebayor kueleza sababu ya kuondoka kwake City Of machester hazihusiani na dhana za mashabiki wengi ulimwenguni ambao walidhani huenda ana ugomvi na meneja wa Man City Roberto Mancini, hii leo meneja huyo amevunja ukimya ya kueleza yaliyo moyoni mwake juu ya mchezaji huyo.

Mancini amezungumza masuala hayo alipokutana na mwaandishi wa habari ambao walitaka kufahamu nini mustakabali wake kwa Emmanuel Adebayor mara baada ya kumpeleka kwa mkopo huko Estadio Stantiago Bernabeu yalipo makao makuu ya klabu ay Real Madrid.

Mancini amesema bado ana mapenzi ya dhati na mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 26 na angependa amuone tena katika kikosi chake akiwa tofauti na alivyokua kabla ya kumpelea Real Madrid kwa mkopo siku mbili zilizopita.

Amesema mashabiki wengi ulimwenguni wamekua wakimuona yeye mbaya juu ya suala la Adebayor lakini ukweli ni kwamba anamuhusudu mchezaji huyo na wala hakumpelekea kwa mkopo huko nchini Hispania kwa minajili ya shari bali amefanya hivyo kwa kutaka kumuongezea makali.

Mtaliano huyo pia ameeleza wazi kwamba ugomvi kati ya Emmanuel Sheyi Adebayor pamoja na Habib Kolo Toure uliojitokeza majuma matatu yaliyopita, wakiwa mazoezini nao hauhusiani na safari hiyo ya mkopo hivyo amewataka mashabiki kuwa watulivu na kuitazama Man city kwa mazuri zaidi.

Kauli ya Mancini imetoka baada ya Adebayor kuzungumza kwa mafumbo huko mjini Madrid alipokuwa katika mkutano wa kutambulishwa kwa waandishi wa habari, ambapo alisema safari ya mjini humo inafungua maisha mapya kwake na kufunga mabalaa yaliyomuandama toka mwanzoni mwa mwaka 2010 pale timu ya taifa lake la Togo ilipovamiwa katika mji wa Kabinda ikiwa safarini kuelekea kwenye fainali za mataifa ya bara la Afrika zilizofanyika nchini Angola.

Wakati huo huo Mancini amesema mara baada ya kumtoa kwa mkopo Emmanuel Sheyi Adebayor, pia huenda akamtoa kwa mkopo Michael Johnson ambae anahitaji kucheza kwa ajili ya kuendelea kumshawishi kocha mkuu wa timu ya taifa ya Uingereza Fabio Capello ili aweze kumuita katika kikosi chake, huku akikataa kumtoa kwa mkopo Shaun Wright Philips ambae tayari alikua ameshaanza kuhusishwa na taarifa za kutaka kujiunga na Fulham.

No comments:

Post a Comment