KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Saturday, January 29, 2011

NI MORROCO !!!


Hatimae fumbo la nani atakuwa mwenyeji wa fainali za mataifa ya bara la Afrika hii leo limefumbuliwa huko mjini Lumbumbashi, Jamuhuri ya kidemokrasia ya Kongo, baada ya wajumbe wa kamati ya utendaji ya CAF kupiga kura.

Fumbo hilo limefumbuliwa huku mataifa mawili pekee ndio yaliyojitiokeza kuwania nafasi hiyo ambayo imeangukia kwa nchi ya Morocco huku nchi ya Afrika kusini ikiambulia bahati ya kuwa mwenyeji wa fainali hizo kwa mwaka 2017.

Nchi ya Morocco imepata nafasi hiyo kwa mara ya kwanza baada ya kuandaa fainali hizo kwa mara ya mwisho mwaka 1988 ambapo bingwa wa fainali za mataifa ya Afrika kwa mwaka huo alikuwa Cameroon kufuatia kisago cha bao moja kwa sifuri walichokitoa kwa timu ya taifa ya Nigeria.

Mara baada ya nchi ya Morocco kutangazwa kuwa mshindi wa kuandaa fainali za mataifa ya Afrika mwaka 2015, muwakilishi wan chi hiyo Ali Fassi Hihiri alitoa shukurani za dhati kwa niaba ya viongozi wa chama cha soka cha nchi hiyo kwa wajumbe wa kamati ya utendaji ya CAF kwa kuipatiwa nafasi hiyo pekee nchi yao.

Amesema watajitahidi kufanya maandalizi makubwa ili kuzifanya fainali za mwaka huo kuwa utofauti mkubwa zaidi ya zile zilizopita na zitakazofanyika mwaka ujao huko Equatorial Guinea kwa kushirikiana na nchi ya Benin.

Nae raisi wa chama cha soka nchini Afrika kusini Kirsten Nematandani amekubaliana na matokeo ya kura zilizopigwa na kudhirisha kwamba wamefurahishwa na hatua ya kupata nafasi ya kuwa wenyeji wa fainali za bara la Afrika za mwaka 2017.

Afrika kusini tayari wameshawahi kuwa wenyeji wa fainali za mataifa ya bara la Afrika za mwaka 1996, ambazo zilishuhudia wenyeji wakitawazwa kuwa mabingwa baada ya kuichapa timu ya taifa ya Tunisia mabao mawili kwa sifuri.

Hii si mara ya kwanza kwa nchi za Morocco na Afrika kusini kukutana katika kinyang’anyiro cha kutaka kuwa mwenyeji wa fainali za soka, kwani kama itakumbukwa vyema nchi hizo zilionyeshana upinzani mkubwa wa kutaka kuandaa fainali za kombe la dunia za mwaka 2010, na matokeo yalipotangazwa nchi ya Afrika kusini iliibuka kinara kwa kupata kura 14 dhidi ya 10.

Wakati huo huo kamati ya utendaji ya CAF pia imefanya maamuzi ya kuipa nafasi nchi ya Morocco kuwa mwenyeji wa fainali za mataifa ya Afrika chini ya umri wa miaka 17 za mwaka 2013 huku nchi ya Rwanda ikiambulia nafasi ya kuandaa fainali za mataifa bingwa barani humo (CHAN) za mwaka 2016.

No comments:

Post a Comment