Kiungo wa kimataifa toka nchini Mali Mahamadou Diarra anajiandaa kuondoka huko Estadio Stantiago Barnabeu katika kipindi hiki cha dirisha dogo la usajili huku taarifa zikieza kwamba kiungo huyo yu njiani kurejea nchini Ufaransa kujiunga na klabu ya As Monaco.
Mahamadou Diarra mwenye umri wa miaka 29 anajiandaa na safari hiyo baada ya kukosa nafasi katika kikosi cha meneja Jose Mourinho ambacho kimekua na mabadiliko makubwa toka alipowasili klabuni hapo mwezi May mwaka 2010.
Kiungo huyo aliejiunga na klabu ya Real Madrid mwaka 2006, hii leo alitarajiwa kupimwa afya yake huko mjini Monaco kabla ya kuketi chini na viongozi wa klabu hiyo na kukubaliana namna ya kusaini mkataba ambao utamuwezesha kurejea katika mikiki mikiki ya ligi ya nchini Ufaransa.
Wakati kiungo huyo akiwa katika utaratibu huo, vyombo mbali mbali vya habari mjini Madrid nchini Hispania pamoja na mjini Monaco nchini ufaransa vimeripoti kwamba tayari viongozi wa Real Madrid na wale wa As Monaco wameshaketi chini na kumaliza utaratibu wa uhamisho wa mchezaji huyo.
Mahamadou Diarra kabla hajaondoka nchini ufaransa na kuelekea nchini Hispania alikua akiitumikia klabu ya Olympic Lyon ambayo aliichezea michezo 123 na kufanikiwa kupachika mabao sita.
No comments:
Post a Comment