KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Monday, January 3, 2011

Alan Pardew ASHINDWA KUELEZA WAZI JUU YA BECKHAM.


Meneja wa klabu ya Newcastle Utd Alan Pardew amesema inamlazimu kufanya usajili wa kiungo mshambuliaji katika kipindi hiki cha dirisha dogo la usajili kilichoanza siku mbili zilizopita.

Alan Pardew ameweka wazi mkakati huo usiku wa kuamkia hii leo ambapo amesema angependa kufanya hivyo kwa lengo la kukiongezea nguvu kikosi chake kilichorejea kwenye ligi kuu ya soka nchini Uingereza msimu huu.

Meneja huyo aliechukua mikoba klabuni hapo mara baada ya kutimuliwa kazi kwa Criss Hughton amesema lengo lake kubwa ni kumpata mchezaji mwenye uwezo kama kiungo wa kimataifa toka nchini Uingereza pamoja na klabu ya LA Galax ya nchini Marekani David Beckham lakini alipotakia kuthibitisha kama kweli anamuhitaji mchezaji huyo pasipo
kumfananisha alitafuna maneno na kushindwa kusema ukweli juu ya suala hilo.

Amesema hadhani kama klabu yake inashindwa kumsajili mchezaji huyo, baada ya kuwasilisha mambo yake ya kufanya hivyo kwa viongozi wa ngazi za juu huko St James Park.

No comments:

Post a Comment