KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Monday, January 3, 2011

BECKHAM ATAICHEZEA SPURS KWA MIEZI MITATU !!


Wakati Pardew akishindwa kueleza wazi juu ya David Beckham huko White Hert Lane mambo yapo shwari kwa meneja wa klabu ya Tottenham Hotspurs Harry Redknapp ambapo ameendelea kutamba kumsajili kiungo huyo mwenye umri wa miaka 35.

Amesema Beckham atajiunga nao kwa kipindi cha miezi mitatu ijayo na tayari wameshafanya mawasilino na uongozi wa klabu yake ya LA Galax ambapo mawasiliano hayo yanaendelea vyema mpaka sasa.

Amesema endapo dili hilo litakamilika, kikosi chake kilichosheheni wachezaji wenye damu changa kitajifunza mengi kutoka kwa mchezaji huyo ambae amekua mfano kwa wachezaji wengi chipukizi ulimwenguni kote.

No comments:

Post a Comment