Kocha mkuu wa timu ya taifa ya Jamuhuri hiyo Cho Kwang-rae ametoa taarifa za kustahafu soka kwa kiungo mshambuliaji wa klabu ya Manchester United Park Ji-sung ambae alikua ni miongoni mwa wachezaji wake walioshiriki kwenye fainali za mataifa ya bara la Asia ambazo hii leo zimefikia tamati.
Kocha huyo amethjibitisha taarifa hizo baada ya kikosi chake kuambulia nafasi ya tatu kwenye fainali hizo kufuatia kuifunga timu ya taifa ya Uzbekistan mabao matatu kwa mawili katika mchezo uliofanyika jana nchini Qatar.
Cho Kwang-rae amesema mchezaji huyo alimuarifu taarifa za kutaka kustahafu soka la kimataifa kabl ya mchezo huo wa jana nay eye bina khiyana alikubaliana na msimamo wake ambao amedai ni wa busara tena wenye kutaka kutoa nafasi kwa wachezaji wengine chipukizi ndani ya kikosi chake.
Amesema mbali na Park Ji Sung pia mlinzi wa pembeni wa klabu ya Al hilal ya nchini Saudi Arabia Lee Young-pyo mwenye umri wa miaka 33 amefikia maamuzi ya kustafu soka la kimataifa.
Lee Young-pyo ambae tayari ameitumikia klabu ya Tottenham Hotspurs ya nchini Uingereza mwaka 2005-2008 amefikia maamuzi hayo huku akieleza wazi kwamba kwa sasa anataka kuelekezea nguvu zake kwenye klabu yake ambayo kwa sasa inatetea ubuingwa wa ligi ya nchini Saudi Arabia.
Park Ji Sung ametangaza kustahafu soka la kimataifa hukua kiacha kumbu kumbu ya kuitumikia timu ya taifa ya jamuhuri ya watu wa Korea michezo 100 na kupachika mabao 13.
Kwa upande wa Lee Young-pyo ameitumikia timu ya taifa lake michezo 123 na kufunga mabao 5.
No comments:
Post a Comment