KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Monday, January 3, 2011

ANGOLA WACHEZEA KICHAPO FALME ZA KIARABU.


Kikosi cha timu ya taifa ya Angola kimeanza vibaya ziara ya huko Falme za kiarabu baada ya kukubali kisago cha bao moja kwa sifuri kilichotolewa na kikosi cha timu ya taifa ya Iran katika mchezo wa kimataifa wa kirafiki uliochezwa mjini Doha nchini Qatar.

Kikosi cha timu ya taifa ya Angola ambacho kwa sasa kinajiandaa na fainali za mataifa bingwa barani Afrika CHAN zitakazofanyika mwezi ujao nchini Sudan, kilijikuta kikibamizwa bao hilo pekee kupitia kwa mshambuliaji wa timu ya taifa ya Iran Javad Nekounam.

Javad Nekounam alipachika bao hilo la ushindi baada ya kutumia udhaifu wa mabeki wa timu ya taifa ya Angola kwa kuunganisha kwa kichwa mpira wa kona.
Kikosi cha timu ya taifa ya Angola *The Palancras Negras* kitarejea tena uwanjani kupambana na timu ya taifa ya Saudi Arabia katika mchezo mwingine wa kimataifa wa kirafiki.

Timu za taifa za Iran pamoja na Saudi Arabia nazo zinajiandaa na fainali za mataifa ya barani Asia ambazo zitaanza kuunguruma January saba mwaka huu.

Wakati timu ya taifa ya Angola ikianza vibaya michezo yake ya kujipima nguvu huko falme za kiarabu, kikosi cha timu ya taifa ya Zambia hii leo kimerejea nyumbani kikitokea nchini Misri katika jiji la Cairo kilipokua kikicheza mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya Kuwait.

Zambia wamerejea nyumbani huku wakiwa na kumbu kumbu ya kupoteza mchezo huo kwa idadi ya mabao manne kwa sifuri, huku kocha mkuu Dario Bonetti akiwaahidi waandishi wa habari kuyafanyia kazi makosa yaliyopelekea kupokea kisago hicho kizito.

Timu ya taifa ya Kuwait nayo imeutumia mchezo huo wa kirafiki kama sehemu ya kujiandaa na fainali za mataifa ya barani Asia.

No comments:

Post a Comment