Meneja wa klabu ya man Utd Sir Alex Ferguson ametoa msimamo wake katika kipindi hikli cha usajili wa dirisha dogo kwa kusema hatomsajili mchezaji yoyote.
Sir Alex Ferguson mwenye umri wa miaka 69, amesema kikosi chake kinamridhisha kufanya maamuzi hayo kutokana na uwezo mkubwa ulioonyeshwa na wachezaji wake toka mwanzoni mwa msimu huu, hivyo haoni sababu ya kukiongezea nguvu.
Amesema licha ya kupanga mpango wa kutokufanya usajili, anategemea kumuuza kwa mkopo mshambuliaji wake wa kimataifa toka nchini italia Federico Macheda ambae ameshindwa kujihakikishia nafasi kwenye kikosi cha kwanza.
Amesema anatarajia kufanya hivyo kwa lengo la kutaka kumuiongezea ufanisi wa kiuchezaji mshambuliaji huyo ambae huenda akarejea nchini kwao Italia kujiunga na klabu ya SS Lazio au AS Roma ama kuendelea kubaki nchini Uingereza kwa kusajiliwa na Bolton Wanderers.
Ferguson pia amethibitisha kwamba wachezaji wake wengine wawili aliowauza kwa mkopo mwanzoni mwa msimu huu kama Danny Welbeck anaeitumikia klabu ya Sunderland pamoja na Mame Biram Diouf, anaeitumikia klabu ya Blackburn Rovers wataendelea kuvuchezea vilabu hivyo hadi mwishoni mwa msimu huu.
No comments:
Post a Comment