KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Monday, January 3, 2011

Carlo Ancelotti BADO ANA MATUMAINI NA KIKOSI CHAKE.


Meneja wa klabu bingwa nchini Uingereza Chelsea Carlo Ancelotti ameendelea kutoa msisitizo wa kikosi chake kutetea taji la ligi msimu huu licha ya kurejea kwenye mwenendo wa kusua sua baada ya matokeo ya sare ya mabao matatu kwa matatu dhidi ya Aston Villa hapo jana.

Carlo Anceloti ametoa msisistizo huo huko Stamford Bridge jijini London yalipo maskani makuu ya klabu ya Chelsea ambapo amesema haoni sababu ya kukiondoa kikosi chake katika mbio za ubingwa msimu huu ili hali habo kuna nafasi kubwa ya kufikia malengo aliyojiwekea.

Amesema tofauti ya point sita iliopo kati yao na vinara wa ligi hiyo Man utd sambamba na Man city wenye point 41 kila mmoja, bado hakumfanyi ahofie huenda ubingwa walio nao mikononi kwa sasa unaweza kupotea, bali kazi kubwa waliyonayo hivi sasa ni kuhakikisha wanarejea katika hali ya ushindi.

Mzee huyo mwenye umri wa miaka 51 amebainisha kwamba kwa asilimia kubwa kikosi chake kimekua kikicheza chini ya kiwango na suala hilo ndilo linasababisha matokeo mabovu yanayopatikana lakini akaonyesha imani kwamba wachezaji hao watarejea katika hali zao za kawaida kama ilivyokua mwanzoni mwa msimu huu.

Hata hivyo Carlo Anceloti ameeleza wazi kusikitishwa kwake na matokeo ya mchezo wa jana ambao ulishuhudia mabao sita yakifungwa kwenye uwanja wa Stamford Bridge huku kikosi chake kikigawana point moja na wageni Aston Villa.

Amesema tayari wachezaji wake alionyesha uwezo wa kuumuidu mchezo huo baada ya kusawazisha makosa yao yaliyopelekea kuwa nyuma kwa idadi ya mabao mawili kwa moja, lakini cha kushangaza katika dakika za lala salama matokeo yalibadilika kufuatia uzembe uliofanywa na wachezaji wake wa safu ya ulinzi.

No comments:

Post a Comment