Mabingwa watetezi wa ligi kuu ya soka nchini Uingereza Chelsea, bado wanaendelea na utaratibu wa kutaka kumsajili beki wa kimataifa toka nchini Brazil na klabu ya Benfica ya nchini Ureno David Luiz Moreira Marinho.
Utaratibu wa kusajiliwa kwa beki huyo umethibitishwa na meneja wa klabu hiyo ya jijini London Carlo Michelangelo Ancelotti mara baada ya mchezo wa jana dhidli ya Bolton ambapo amesema bado wanajitahidi kukamilisha mazungumzo kati yao na viongozi wa klabu ya Benfica.
Amesema hakuna kilichobadilika mpaka sasa zaidi, ya taratibu za kumaliza mazungumzo ambayo anaamini yatakamilishwa na ada ya uhamisho wa mchezaji huyo ambayo tayari imeshatajwa kuwa ni paund million 17.
Kabla ya kupunguzwa kwa ada hiyo, uongozi wa klabu ya Benfica uliwataka viongozi wa klabu ya Chelsea kutoa kiasi cha paund million 25.5 ambacho kilitajwa kama ada ya uhamisho wa David Luiz mwenye umri wa miaka 23.
No comments:
Post a Comment