KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Saturday, January 15, 2011

David Beckham AMKUNA BABU REDKNAPP.


Meneja wa klabu ya Tottenham Hotspurs Harry Redknapp amesema nafurahishwa na mwenendo wa kiungo wa kimataifa toka nchini Uingereza na klabu ya Los Angel Galaxy a nchini Marekani David Beckham ambae anafanya mazoezi na kikosi chake kwa sasa.

Redknapp amesema kiungo huyo mwenye umri wa miaka 35, amepeleka uhamisichaji mkubwa kwa wachezaji wake ambao amedai wanajifunza mengi kutoka kwa baba huyo wa watoto watatu.

Amesema kila mmoja anamuheshimu Beckham, wanapokua mazoezini na nje ya mazoezi hali ambayo amaifurahia na amebainisha italeta mshikamano wa hali ya juu ambao utakiletea mafanikio kikosi chake msimu huu.

Kabla ya kukubali kufanya mazoezi na kikosi cha klabu hiyo, uongozi Spurs ulikua tayari kumsajili kiungo huyo katika kipindi hiki cha dirisha dogo la usajili lakini, ukata wa fedha za kumlipa mshahara wake kwa juma umekua chanzo cha kushindwa kufanikiwa kwa zoezi hilo.

No comments:

Post a Comment