Siku moja baada ya meneja wa klabu ya Liverpool Kenny Dalglish kutangaza kubadili mawazo ya kumuuza winga wa kimataifa toka nchini Uholanzi Ryan Babel, saa kadhaa zilizopita winga huyo ametoa kauli ya kukubalia kuondoka klabuni hapo kwa minajili ya kujiunga na klabu ya Hoffenheim ya nchini Ujerumani.
Ryan Babel mwenye umri wa miaka 24 amekubalia kuelekea nchini Ujerumani, huku mpaka sasa ikiwa bado haijafahamika nini kinagaubaga cha Kenny Dalglish kutangaza kubadili msimamo wake wa kumuuza winga huyo ambae kwa sasa hapati nafasi ya kucheza katika kikosi cha kwanza.
Hata hivyo siku kadhaa zilizopita uongozi wa klabu ya Hoffenheim ya nchini Ujerumani uliripotiwa kukubali kulipa ada ya uhamisho wa winga huyo lakini jana taarifa zilizotolewa na meneja huyo wa kimataifa toka nchini Scotland zilieleza kwamba dili la uhamisho wa Babel limevunjika.
Ryan Babel alijiunga na klabu ya Liverpool mwaka 2007, akitokea nchini kwao Uholanzi alipokua akiitumikia klabu ya Ajax Amsterdam ambayo ilikubalia kumuza kwa ada ya uhamisho wa paund million 10.
Babel anajiandaa kuondoka Anfiled huku akiwa na kumbu kumbu ya kutozwa fainali ya paund 10,000 na chama cha soka nchini Uingereza, baada ya kukutwa na hatia ya kumdhalilisha muamuzi Howard Webb kufuatia picha ya kutengeneza aliyoiweka kwenye ukurasa wake wa mtandao wa Twiter saa chache baada ya mchezo wa kombe la FA kati ya Liverpool dhidi ya Man utd uliochezwa mwanzoni mwa mwezi huu kumalizika huko Old Trafford ambapo majogoo wa jiji waliambulia kichapo cha bao moja kwa sifuri.
No comments:
Post a Comment