Raisi wa chama cha soka nchini Gambia Seedy Kinteh ameonyesha kumuunga mkono raisi wa chama cha soka nchini Ghana Kwesi Nyantakyi katika harakati za kuwani nafasi ya ujumbe wa kamati ya utendaji ya shirikisho la soka barani Afrika CAF.
Seedy Kinteh ameonyesha hali hiyo baada ya kukiri kwamba Kwesi Nyantakyi ni mtu sahihi anastahili kushinda nafasi hiyo kwenye uchaguzi mkuu wa CAF ambao utafanyika mara baada ya mkutano mkuu wa 33 wa shirikisho hilo mjini Khartoum nchini Sudan siku mbili kabla ya mchezo wa hatua ya fainali ya michuano ya mataifa bingwa barani Afrika CHAN ( Februari 23).
Raisi huyo wa soka nchini Gambia ambae ni mmoja wa watu wanaompigia kampeni Nyantakyi ili aweze kufanikiwa kuwa mjumbe wa kamati ya utendaji ya CAF, ameongeza kwamba licha ya kuwa mwana kampeni bado anakubaliana na hali halisi ya uongozi wa mtu huyo kutoka Ghana ambae amekiri ni mmoja wa viongozi walioipa sifa kubwa nchi ya Ghana katika tasnia ya soka pamoja na bara zima la Afrika.
Wapinzani wa Kwesi Nyantakyi katika kinyang’anyiro cha kuwania nafasi ya ujumbe wa CAF ukanda wa Afrika ya magharibi wanatoka nchini Benin, Niger pamoja na Togo.
No comments:
Post a Comment