Menyekiti wa klabu ya Tottenham Hotspurs Daniel Levy ameendelea kueleza mikakati ya kuyahamisha makazi ya klabu hiyo katika uwanja mpya na kuiondoa katika makao ya sasa yaliopo huko White Hert Lane kaskazini mwa jiji la London.
Daniel Levy ambae anapingana vikali na baadhi ya mashabiki wa klabu hiyo amesema uongozi wake umejipanga kufanya jitihada za kuhamisha makazi hayo hata kama ombi lao la kutaka kuumiliki uwanja wa Olympic litashindikana bado mikakati ya kuhama itakuwa pale pale.
Amesema kimtazamo tayari klabu hiyo imeshakua na mashabiki wengi hivyo kuna kila namna ya kuwawezesha kuifuatilia timu yao kwa nafasi, tena wakiwa katika uwanja mkubwa na si uwanja wa sasa wa White Hert Lane ambao una uwezo wa kuchua mashabiki 36, 310 walioketi.
Mashabiki wanaopingana na uongozi wa Daniel Levy wamekua wakihoji kwa nini uongozi huo umetuma maombi ya kutaka kuumiliki uwanja wa Olympic ili hali tayari mradi wa kujenga uwanja mpya wa klabu hiyo ujulikanao kama Northumberland Development Project ulishatangazwa miaka miwili iliyopita.
Katika maelezo ya mradi huo uwanja huo mpya wa klabu ya Spurs unategemea kuwa na uwezo wa kuchukua mashabiki 56,250.
Ikumbukwe kuwa ombi la Spurs kutaka kuumiliki uwanja wa Olympic lipo katika mashaka makubwa kupitishwa na kamati ya michuano ya Olympic ya mwaka 2012 kufuatia mkakati wa kutaka kuondoa sehemu ya kukimbilia endapo watashinda ombi hilo, ili hali West Ham Utd waliowasilisha mambo kama hayo wanapewa nafasi kubwa ya kushinda kutokana na mkakati wa kutoondoa sehemu ya kukimbilia ya uwanja huo.
No comments:
Post a Comment