KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Saturday, January 1, 2011

BECKS KUJIUNGA NA SPURS.



Ikiwa ni siku ya kwanza ya msimu wa dirisha dogo la usajili, meneja wa klabu ya tottenham Hotspurs Harry Redknapp, ametangaza hadharani kuwa kwenye mkakati mkali wa kutaka kumsajili kwa mkopo kiungo wa kimataifa toka nchini Uingereza pamoja na klabu ya LA Galax David Beckham.

Redknapp ametangaza mkakati huo katika mkutano na waandishi wa habari uliokua unazungumzia mchezo wa hii leo ambapo Spurs wameonyeshana shughuli pevu na Fulham huko White Hert Lane.

Amesema atajaribu kutuma ofa ya kumsajili kwa mkopo huko nchini Marekani kiungo huyo ambae alikua nahodha wa timu ya taifa ya Uingereza na ana matumaini na uongozi wa klabu ay LA Galax kumkubalia suala hilo.

Beckham mwenye umri wa miaka 35, kwa sasa kikosi cha klabu yake kipo kwenye mapumziko kikisubiri kuanza kwa msimu mpya wa ligi ya nchini marekani ambao unataanza kutimua vumbi lake March 15 mwaka huu.

Hii so mara ya kwanza kwa David Beckham kurejea barani Ulaya kucheza soka kwa mkopo ambapo kama itakumbukwa vyema mwaka 2009 na 2010, kiungo alisajiliwa kwa mkopo na klabu ya AC Milan.

No comments:

Post a Comment