Hakika kila siku ya mwaka 2010 ilipokua ikirejea kwake Jalali nilikua namshukuru kwa kuniwezesha kuwa na afya njema na kunifungulia rizki yangu pamoja na kwa wale wanaonizunguuka hilo kubwa kwake Jalali ninarejesha shukurani kwa mikono miwili kama alivyotuagiza katika vitabu vinavyotuongoza kiimani.
Nilipokosea nilijuta na kumuomba Jalali nisirejee tena pale nipokosea, hali kadhalika nilipomkosea yoyote nilimtaka radhi kama kuna yoyote sikumtaka radhi naomba anisamehe sasa kwani lengo langu ni kuuanza mwaka 2011 bila kuwa na doa la matatizo na yoyote yule.
Walionikosea nimewasamehe pia lakini kama kusamehewa zaidi ya yale makosa yaliyonikwaza hadi nikashindwa kutimiza malengo yangu ninamuachia mwenyezi najua atamsamehe yoyote alienitenda hadi kufikia hatua hiyo.
Nilijitahidi kufanya jitihada zangu za kusaka maisha naimani nilichojaaliwa ndicho mungu alichonipangia kwa mwaka 2010, na imani yangu yanituma yapo mengi mazuri amenipangia kwa mwaka 2011 tena zaidi ya haya niliyofanikiwa, lakini pale niliposhindwa bado naamini mungu hakutaka hivyo.
Nakushukuru wewe ulienipa sapoti ya kutembelea blog yangu kila mara na nina imani umeyafurahia yote niliyo kuletea kama habari kwa mwaka 2010, ninakuahidi panapo uhai mwenyezi akipenda mengi zaidi yanakuja kwa mwaka 2011.
Mwenyezi atulinde sote kwa kheri na atuepushe na shari za wale wadogo na wakubwa katika ulimwengu huu.
Naimani tutaendelea kuwa pamoja, endelea kuitembelea blog yako ya viwanja.blogspot.com
Kaka ulilofanya ni zaidi ya uungwana.
ReplyDeleteUmeonesha kuwa wewe waangalia mbele na kwa PAMOJA tutaweza kusonga
Nimekuwa nikijivunia mtazamo wako wa mambo na hili lazidi "shindilia" msumari wa heshima kwako
BLESSINGS