KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Friday, January 28, 2011

BLACKPOOL KUKATA RUFAA?


Siku moja baada ya chama cha soka nchini Uingereza FA, kutangaza kuitoza fainali klabu ya Blackpool kufuatia kosa la kuwachezesha wachezaji wa kikosi cha pili kwenye mchezo wa ligi dhidi ya West Ham Utd uliochezwa Novemba 10 mwaka jana, metandaji mkuu wa klabu hiyo Karl Oyston amezungumzia suala hilo.

Karl Oyston amezungumzia suala hilo huku akionyesha dalili zote za klabu hiyo kuwa tayari kukata rufaa ya kupinga adhabu ya kulipa faini ambayo tayari ilishapingwa na meneja mkuu wa kikosi chao Ian Holloway siku moja baada ya kitendo hicho kujitokeza huko Villa Park.

Amesema tayari wameshapokea taarifa rasmi kutoka ndani ya chama cha soka nchini Uingereza FA inayowataka kulipa fainali hiyo, lakini kwa sasa wanalijadili suala hilo katika kikao cha bodi na ana imani wataibuka na azimio la kukata rufaa.

Oyston pia amesisitiza jambo la kukaa meza moja na meneja wao Ian Holloway ambae alitangaza kujiuzulu endapo klabu hiyo itaadhibiwa na FA kwa kosa la kuwachezesha wachezi wa kikosi cha pili kwenye mchezo wa ligi kuu.

Amesema lengo kubwa la kukaa na meneja huyo ni kutaka kumsihi asitimize azma yake ya kujizulu, kwani endapo atafanya hivyo ataiacha klabu hiyo kwenye kipindi kigumu cha kushindwa kutimiza malengo waliyojiwekea msimu huu.

Kama itakumbukwa vyema siku moja baada ya mchezo kati ya Blackpool dhidi ya Aston villa kuchezwa Novemba 10 mwaka jana Ian Holloway alitoa kauli kwa ukali ya kuchukizwa na sheria za ligi kuu, ambazo zinawafanya mameneja kushindwa kutimiza malengo yao ya kuwatumia baadhi ya wachezaji wanaowasajili.

Katika mchezo huo Aston Villa walifanikiwa kupata ushindi wa mabao matatu kwa mawili.

No comments:

Post a Comment