KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Wednesday, January 12, 2011

CAF YAKAZIA MSIMAMO WAKE.


Shirikisho la soka barani Afrika CAF limeendelea na msimamo wake wa kuifungia klabu bingwa nchini Tunisia Esperance, ya kucheza michezo miwiwli ya kimataifa iliyo chini ya shirikisho hilo bila ya kuwa na mashabiki.

CAF wameendelea kukazia msimamo huo kufuatia rufaa iliyowasilishwa na uongozi wa klabu hiyo ya kupinga adhabu iliyotoplewa mwezi Novemba mwaka jana baada ya mchezo wa pili wa hatua ya fainali ya ligi ya mabingwa barani Afrika dhidi ya TP Mazembe.

Kitendo cha kufungiwa kwa mashabiki kutokuingia uwanjani wakati Esperance wakicheza nyumbani kwenye michezo ya kimataifa, kilisababishwa na baadhi ya mashabiki kung’oa viti na kuvirusha uwanjani hali ambayo ilihatarisha usalama wa wachezaji.

Kwa kitendo hicho CAF pia uliutaka uongozi wa klabu hiyo ya nchini Tunisia kulipa faini ya dola za kimarekani 52,500.

Mbali na sakata hilo pia shirikisho hilo la soka barani Afrika limetoa msisistizo wa kuendeleza adhabu ya kumfungia kiungo wa klabu Espirance Aymen Ben Amour kutokucheza michezo sita ya kimataifa sambamba na kulipa faini ya dola za kimarekani 10,000.

Aymen Ben Amour alikumbwa na adhabu hiyo, baada ya kumtemea mate mchezaji wa TP Mazembe katika mchezo wa hatua ya fainali, kitendo ambcho kilimlazimu muamuzi kumuonyesha kadi nyekundu.

Kabla ya kufanywa kwa kosa hilo katika mchezo wa fainali, tayari CAF walikua wameshaiadhibu klabu ya, Esperance kwa kuitoza faini ya dola za kimarekani 65,000 kufutaia wachezaji wake kuonyesha vitendo vya utovu wa nidhamu mbele ya wachezaji wa klabu ya Al Ahly ya nchini Misri walioiondosha kwenye hatua ya nusu fainali.

No comments:

Post a Comment