KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Wednesday, January 12, 2011

Goran ‘Plavi’ Stevanovic ATUA JIJINI ACCRA.


Kocha wa kimataifa toka nchini Serbia Goran ‘Plavi’ Stevanovic hii leo amewasili mjini Accra nchini Ghana kwa ajili ya kuanza mazungumzo ya kusaini mkataba wa kukinoa kikosi cha timu ya taifa hilo.

Kocha huyo amewasili nchini humo baada ya uongozi wa chama cha soka nchini Ghana kumtangaza kuwa kocha mtarajiwa kufuatia kushinda vigezo vilivyotakiwa na uongozi wa GFA.

Goran ‘Plavi’ Stevanovic mwenye umri wa miaka 44 anategemea kuanza mazungumzo hayo huku shughuli kubwa iliyo mbele yake ni kuhakikisha kikosi cha Black Stars kinapata nafasi ya kucheza fainali za mataifa ya Afrika kwa maka 2012 na 2013.

Tayari uongozi wa GFA umeshatangaza kuwa mchezaji huyo wa zamani wa klabu ya Osasuna ya nchini Hispania ataanza kazi rasmi ya kukinoa kikosi cha timu ya taifa iliyoachwa na Milovan Rajevac tarehe mosi mwezi February huku mshahara wake ukitarajiwa kuwa Euro elfu 30 kwa mwezi.

No comments:

Post a Comment