KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Tuesday, January 11, 2011

Ronaldinho Gaucho ARUDI NYUMBANI.


Hatimae kiungo mshambuliaji toka nchini Brazil Ronaldinho Gaucho, amerejea nyumbani na kujiunga na klabu ya Flamengo ya mjini Rio de Janeiro na kukata ngebe za klabu ya Blackburn Roves ya nchini Uingereza ambayo ilikua mstari wa mbele katika harakati za kutaka kumsajili katika kipindi hiki cha mwezi januari.

Ronaldinho mwenye umri wa 30 amerejea nyumbani kujiunga na klabu ya Flamengo baada ya kupewa Baraka zote na uongozi wa klabu ya Ac Milan iliyomsajili akitokea Fc Barcelona mwaka 2008.

Tayari uongozi wa klabu ya Blackburn Roves kupitia kwa meneja wao w amuda Steve Kean walikua wameshatangaza kutenga kiasi cha paund million 20 kwa ajili ya kumsajili kiungo huyo lakini mvutano ulijitokeza baina yao na klabu ya Gremio na Palmeiras zote za nchini Brazil kutangaza kuhitaji saini yake.

Licha ya mvutano huo kujiri kwa muda, bado klabu ya Flamingo ilikua ikimfuatilia Ronaldinho kwa ukaribu zaidi nah ii leo wamefanikisha utaratibu wa kumrejesha katika radhi ya nyumbani ambayo aliiacha toka mwaka 1998.

Akimtambulisha mbele ya waandishi wa habari raisi wa klabu ya Flamengo Patricia Amorim amesema wamefanikisha suala la kumsajili mchezaji huyo ikiwa ni sehemu ya kutimiza ahadi waliyoitoa kwa mashabiki ambao siku kadhaa zilizopita walielezwa kuna uwezekano wa kusajiliwa kwa mchezaji mashuhuri klabuni hapo.

Kiongozi huyo wa juu wa klabu hiyo ya mjini Rio de Janeiro, pia ametoa shukurani kwa viongozi wenzake pamoja na kwa meneja mjuu Wanderley Luxemburgo kwa ushirikiano mkubwa waliompa kufanikisha suala al usajili wa Ronaldinho.

Wakati kiungo huyo akitambulishwa kwa waandishi wa habari mjini Rio de Janeiro, huko mjini Milan nchini Italia meneja mkuu wa klabu ya AC Milan Massimiliano Allegri ametoa shukurani zake za dhati kwa mchezaji huyo kwa juhudi zake ambazo zimekiwezesha kikosi chake kufika hapa kilipo na amesema katu hatomsahau.

Ronaldinho imemlazimu kuondoka Ac Milan baada ya kupoteza nafasi ya kucheza katika kikosi cha kwanza, hatua mbayo imesababishwa na usajili Zlatan Ibrahimovic pamoja na Robinho mwanzoni mwa msimu huu huku uongozi wa klabu hiyo ikifanya usajili wa Antonio Cassano ndani ya juma hili akitokea Sampdoria.

No comments:

Post a Comment