Thursday, January 20, 2011
CHELSEA WANAJIANDAA KATIKA KILA HALI !!
Beki wa pembani wa kimataifa toka nchini Ureno José Bosingwa da Silva anajiandaa kusaini mkataba mpya wa kuendelea kuitumikia klabu ya Chelsea hadi mwaka 2012.
Beki huyo mwenye umri wa miaka 28, anajiandaa kusaini mkataba mpya kufuatia mkataba wake wa sasa kutarajia kufikia kikomo mwishoni mwa msimu huu huku taarifa zikieleza kwamba tayari kuna baadhi ya vilabu vinataka kumsajili kupitia kipindi hiki cha dirisha dogo.
Hata hivyo imeelezwa kuwa José Bosingwa da Silva ambae ni mzaliwa wa Jamuhuri ya kidemokrasia ya Kongo katika jimbo la Mbandaka, huenda akapewa mkataba wa mwaka mmoja wa kuendelea kubaki jijini London hali ambayo inahofiwa huenda ikamkimbiza klabuni hapo mwishoni mwa msimu huu atakapokua mchezaji huru.
Wakati huo uongozi wa klabu ya Chelsea unaendelea vyema na harakati za kutaka kumsajili beki wa kimataifa toka nchini Brazil pamoja na klabu ya Benfica ya nchini Ureno David Luiz Moreira Marinho.
Chelsea wanaendelea vyema katika harakati hizo, kufuatia uongozi wa klabu ya Benfica kufungua milango ya kuketi meza moja na kuanza kujadili ada ya uhamisho wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23.
Licha ya kuwepo kwa uwezekano wa kufanyika kwa mazungumzo hayo, tayari moja ya gazeti nchini Uingereza mapema hii leo limeripoti kwamba beki huyo huenda akauzwa kwa ada ya uhamisho wa paund million 26, huku uongozi wa klabu ya Man city ukitamani kuingilia dili hilo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment