Hatimae aliekua meneja wa muda wa klabu ya Blackburn Rovers Steve Kean amesaini mkataba unaomuwezesha kutambulika kama meneja kamili wa kikosi cha klabu hiyo yenye maskani yake makuu huko Ewood Park.
Kean, amesaini mkataba wa miaka miwili ambao utamuweka huko Ewood Park hadi mwaka 2013, ambapo bahati hiyo imepatikana mara baada ya kutimuliwa kazi kwa aliekua meneja klabuni hapo Sam Allardyce.
Mwenyekiti wa klabu hiyo mama Anuradha Desai amesema wamefikia maamuzi ya kumkabidhi nafasi hiyo Kean baada ya kuamini anaweza kufikia malengo waliyoyaweka msimu huu na msimu ujao.
Amesema ni vigumu kwa kila mmoja kuelewa nini kilichopelekea maamuzi hayo wakati tayari walishaueleza umma wa mashabiki wa klabu hiyo watatafua meneja mwingine mwishoni mwa msimu huu, lakini ukweli ni kwamba wameridhishwa na kazi ya Steve Kean ambayo kwa sasa ameifanya kwa muda wa majuma manne.
No comments:
Post a Comment