KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Thursday, January 20, 2011

MILANGO LIVERPOOL IWAZI KWA Luis Suarez PAMOJA NA Stewart Downing.


Mwenyekiti wa klabu ya Liverpool Tom Werner amesema uongozi wa klabu hiyo utampatia fedha za kutosha meneja wa kikosi chao Kenny Dalglish kwa ajili ya kufanya usajili katika kipindi hiki cha dirisha dogo kinachoendelea hadi mwishoni mwa mwezi huu.

Tom Werner ametoa kauli hiyo kwa lengo la kuwaondoa hofu mashabiki wa klabu hiyo ambao wanadhani huenda uongozi mpya wa Liverpool hautaki kufanya usajili wa mchezaji yoyote katika kipindi hiki ambacho kikosi chao kinahitaji msaada wa wachezaji wapya.

Amesema tayari wameshaketi chini na Dalglish, na ameshawaeleza nini anachokihitaji ndani ya kikosi chake kwa sasa hivyo siku sio nyingi, mchezaji ama wachezaji wanahitajika klabuni hapo watasajiliwa.

Kwa sasa mchezaji anaezungumzwa sana huenda akajiunga na klabu hiyo ya mjini Liverpool ni mshambuliaji wa kimataifa toka nchini Paraguay pamoja na klabu ya Ajax Amsterdam Luis Suarez pamoja na winga wa kimataifa toka nchini Uingereza na klabu ya Aston Villa Stewart Downing.

Katika hatua nyingine Tom Warner amautetea uongozi mpya wa klabu hiyo kwa kusema haukua na dhamira ya kumtimua kazi yoyote klabuni hapo zaidi ya kuboresha mazingira ambayo yalionekna kuwa madhaifu katika harakati za kuleta maendeleo.

Warner amelizungumnza suala hilo hukub akigusia safari ya aliekua meneja wa kikosi cha Liverpool Roy Hodgson alietimka ndani ya majuma mawili yaliyopita kufuatia matokeo mabovu yaliyokua yakimkabili.

Hata hivyo mwenyekiti huyo wa Liverpool amemtakia Roy Hodgson kila la kheri katika maisha yake baada ya kuondoka Liverpool, na bado wanautambua mchango wake ndani ya klabu hiyo ambayo msimu huu inahofiwa huenda ikashindwa kufikia malengo yaliyowekwa.

Wakati uongozi wa klabu ya Liverpool ukizunguzia upande wake, nae meneja wa klabu hiyo Kanny Dalglish amekiri ni kweli amefanya mazungumzo na mabosi wake na wamemthibitishia suala la kukiongezea nguvu kikosi cha The Reds.

Amesema kwa sasa kubwa lililopo ni kuondoka kwa winga wa kimataifa toka nchini uholanzi Ryan Babel ambae amebakisha asilimia chache kujiunga na klabu ya Hoffenheim ya nchini Ujerumani.

No comments:

Post a Comment