KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Monday, January 17, 2011

Darren Bent KUJIUNGA NA ASTON VILLA ???


Taarifa zinazoihusu klabu hiyo ya Sunderland, ni ombi lililowasilishwa kwa uongozi wa ngazi za juu na mshambuliaji Darren Bent, ambae anataka kuondoka kupitia dirisha dogo la usajili.

Bent ameomba ruhusa hiyo huku akiuhusishwa na taarifa za kutaka kujiunga na klabu ya Aston Villa ambayo ipo tayari kutoa kiasi cha paund million 18.

Hata hivyo taarifa hizo za Daren Bent kuomba uhamisho, zimefanyiwa uchunguzi na shirika la utangazaji la nchini Uingereza BBC, na uliopoulizwa uongozi wa Sunderland umekataa kata kata kulizungumzia suala hilo.

Bent mwenye umri wa miaka 26, alijiunga na klabu ya Sunderland mwaka 2009, akitokea Tottenham Hotspurs kwa ada ya uhamisho wa paund million 10.

No comments:

Post a Comment