KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Monday, January 17, 2011

Thierry Henry AIKUBALI ARSENAL KWA 100%.


Mshambuliaji wa kimataifa toka nchini Ufaransa na klabu ya New York Red Bulls ya nchini Marekani Thierry Henry ameipa nafasi ya kutwaa ubingwa wa nchini Uingereza klabu yake ya zamani ya Arsenal yenye maskani yake makuu jijini London.

Henry ametoa nafasi hiyo kwa klabu ya Arsenal baada ya kufurahishwa na mwenendo wa kikosi cha klabu hiyo msimu huu ambapo amesema unaonyesha uhamasishaji kwa wachezaji ambao amedai wamekomaa kwa sasa.

Mshambuliaji huyo ambae kwa sasa anafanya mazoezi na kikosi cha klabu ya Arsenal amesema haoni sababu ya kuiondoa THE GUNNERS katika mbio za ubingwa msimu huu, wakati tayari dalili zote za uwezekano wa kurejesha heshima ya klabu zimeshaanza kuonekana.

Henry pia ametoa ushauri kwa nahodha na kiungo wa klabu ya Arsenal Cesc Fabregas, ambae anahusishwa na taarifa za kutaka kuondoka klabuni hapo mwishoni mwa msimu huu kwa kumueleza kwamba hana budi kubaki kwa kujinusuru yeye binafsi na kipaji chake kwa ujumla.

Amesema kiungo huyo bado anapendwa na mashabiki wa klabu ya Arsenal na uwezo wake bado unahitajika kwa udi na uvumba hivyo haoni ushauri wa kumpa zaidi ya kumtaka kuendelea kubaki Ashburton Grove.

Thierry Hanry hakuishia hapo bali aliendelea kuipa nafasi kubwa Arsenal katika michuano mingine wanayoendelea kushiriki msimu huu hususan ile michuano ya ligi ya mabingwa barani Ulaya mbapo jeshi hilo la Arsene Wenger litashuka dimbani kupmbana na Fc Barcelona mwezi ujao.

Amesema ana marafiki wengi Barcelona ambao huzungumza nae kila leo na msimu uliopita alipokua akiitumikia klabu hiyo alitamani Arsenel ibamizwe katika hatua ya robo fainali na suala hilo likafanikiwa lakini kwa sasa hana budi kuendeleza mapenzi yake na klabu hiyo ya jijini London kwa kutoa kipaumbele cha kusonga mbele katika mchezo huo wa hatua ya mtoano.

No comments:

Post a Comment