Zimbabwe ni nchi pekee ya barani Afrika iliyowasilisha maombi ya ya kutaka kuwa mwenyeji wa fainali za kombe la dunia za wanawake mwaka 2015.
Taarifa za nchi hiyo kuwasilisha maombi yake huko mjini Zurich nchini Uswiz yalipo makao makuu wa FIFA, zimeshibitishwa na uongozi wa juu wa shirikisho hilo.
Uwezekano wa nchi hiyo ya barani Afrika kushinda katika kinyang’anyiro hicho ni mkubwa kufuatia kuwa na mpinzani mmoja ambae ni nchi ya Canada ambapo hata hivyo yoyote atakaeshindwa katika utaratibu wa kura atapatiwa nafasi ya kipekee ya kuandaa fainali za kombe la dunia za wanawake chini ya umri wa miaka 20 za mwaka 2014.
Fainali za mwaka huu za kombe la dunia kwa wanawake zimepangwa kufanyika nchini Ujerumani kuanzia mwezi June.
Katika hatua nyingine FIFA wamethibitisha kupokea maombi ya nchi nyingine za barani Afrika ambazo ni Ghana na Tunisia zikiomba nafasi ya kuwa wenyeji wa fainali za kombe la dunia za vijana.
Ghana wamewasilisha maombi yao ya kutaka kuwa wenyeji wa fainali za kombe la dunia za vijana chini ya umri wa miaka 17 za mwaka 2013, huku Tunisia ikiwasilisha maombi ya kutaka kuwa mwenyeji wa fainali za kombe la dunia kwa wanawake za vijana chini ya umri wa miaka 20 za mwaka 2015.
Maamuzi rasmi ya nani atakuwa mwenyeji wa fainali za kombe la dunia kwa miaka niliyoitaja yatafanywa Februari 11 mwaka huu baada ya kamati kuu ya FIFA kukutana na kufanya utaratibu wa upigaji wa kura.
No comments:
Post a Comment