Ushauri wa kufanyika kwa fainali za kombe la dunia za mwaka 2022 mwanzoni mwa mwaka, umepingwa vikali na raisi wa shirikisho la soka barani Asia, Mohamed Bin Hammam, na badala yake amesema fainali hizo zitachezwa mwezi June-July kama ilivyo kwa mataifa mengine yaliyowahi kuandaa fainali hizo.
Mohamed Bin Hammam amepinga utaratibu huo baada ya kuzuka kwa mjadala uliodumu kwa kipindi cha mwezi mmoja uliopita ambapo mmoja wa watu waliopendekeza fainali za mwaka huo zifanyike mwezi Januari na si kati kati ya mwaka ni raisi wa shirikisho la soka ulimwenguni kote Sepp Blatter.
Mohamed Bin Hammam amesema nchi kama Qatar bado ina uwezo mkubwa wa kundaa fainali hizo na zikafanyika mwezi June-July kama kawaida na ameahidi kutokuwepo kwa mapungufu yoyote licha ya hofu ya kuwepo kwa joto kali kuendelea kutawala kwenye vichwa vya wanasoka
Katika hatua nyingine raisi huyo wa soka barani Asia pia amepinga ushauri uliotolewa na raisi wa shirikisho la soka barani ulaya, Michael Platin ambao uliutaka uongozi wa chama cha soka nchini Qatar kukubali kusaidiana na nchi za falme za kiarabu kuandaa fainali hizo kwa pamoja ili ziweze kuleta mvuto wa aina yake.
Mohamed Bin Hammam ambae pia ni raia kutoka nchini Qatar amesema haoni sababu ya nchi yao kushirikiana na nchi nyingine katika maandalizi ya fainali hizo za miaka 11 ijayo, ili hali bado wana uwezo wa kutosha pasipo kuhitaji msaada wa nchi nyingine yoyote kutoka ukanda wa falme za kiarabu.
No comments:
Post a Comment