KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Thursday, January 20, 2011

Denilson NA Cesc Fabregas HAWANA BIFU - WENGER.


Baada ya ushindi wa mabao matatu kwa moja uliopatikana usiku wa kuamkia hii leo huko Elland Road, meneja wa klabu ya Arsenal Arsene Wenger, amelazimika kukata mzizi wa fitna na kueleza kiungo wake wa kimataifa toka nchini Brazil Denílson Pereira Neves alikua anamaanisha nini kufuatia kauli yake aliyoitoa mapema hapo jana.

Wenger amesema Denílson Pereira Neves alikua hana nia mbaya kusena Cesc Fabregas ni nahodha wa Arsenal na si kiongozi, bali alimaanisha hakuna aliezaliwa kuwa kiongozi hivyo kila mmoja hujifunza kutokana na mazingira anayoishi.

Amesema wengi walidhani huenda kiungo huyo wa kimataifa wa toka nchini Brazil alimaanisha maana mbaya ambayo inaleta picha ya ugomvi unaoendelea kati yake na Fabregas lakini ukweli ni kwamba Denílson Pereira Neves, alitaka kuufahamisha ulimwengu kwamba Fabregas hakuzaliwa na sifa za uongozi bali amejifunza akiwa ndani ya kikosi cha Arsenal ambacho kwa asilimia kubwa kina vijana wengi.

Arsene Wenger pia amezungumzia kukunwa na kiwango cha kikosi chake ambacho jana kilikua ugenini kikisaka nafasi ya kutinga katika hatua ya nne ya michuano ya kombe la chama cha soka nchini Uingereza FA.

Amesema kiujumla kikosi chake kilicheza vyema na kuthibitisha nini walichokua wakikihitaji kutoka kwa wapinzani wao ambao walikua mbele ya mashabiki wapatao elfu 40 katika uwanja wa Elland Road.

Nae Denílson Pereira Neves alipoulizwa juu ya suala hilo ambalo hii leo lilikua limetapakaa kwenye vyombo mbali mbali vya habari ulimwengu mzima alisema alieleweka vibaya na hakumaanisha kama vyombo vya habari vilivyoandika.

Amesema yeye ni rafiki mkubwa wa Fabregas na mara nyingi wamekuwa wakikaa pamoja kwa lengo la kujifunza mengi katika mchezo wa soka hivyo ni jambo la kipuuzi hii leo akamzungumza vibaya kupitia vyombo vya habari.

Wakati huo huo meneja wa klabu ya Leeds Utd Simon Grayson amekipa tano kikosi chake kwa kuonyesha uwezo wa kutunishiana misuli na klabu kubwa nchini Uingereza nap engine ulimwenguni kote kufuatia upinzani mkali waliouonyesha katika mchezo wa jana.

Amesema wachezaji wake siku hadi siku wamekua wakionyesha mabadiliko makubwa hivyo anaamini juhudi hizo zitawarejesha kwenye ligi daraja la kwanza na ikiwezekana kurejea katika ligi kuu ya soka nchini Uingereza ambayo pia itawarejesha katika michuano ya kimataifa.

No comments:

Post a Comment