KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Thursday, January 20, 2011

FAINALI ZA VIJANA CHINI YA UMRI WA MIAKA 17 AFRIKA.


Fainali za mataifa ya bara la Afrika chini ya umri wa miaka 17 kesho itaendelea tena katika uwanja wa Nyamiorambo nchini Rwanda kwa kushuhudia mchezo wa kumsaka mshindi wa tatu kati ya timu ya taifa ya ivory Coast dhidi ya timu ya taifa ya Congo Brazzaville.

Timu hizo zinakutana hiyo kesho huku zikiwa na kumbu kumbu ya kupangwa katika kundi la pilia mbapo zilizpokutamna katika mchezo wa kundi hilo zilitoka sare ya mabo mawili kwa mawili.

Timu ya taifa ya Congo Brazzaville imefikia hatua ya kucheza mchezo huo wa kesho baada ya kushindwa kufurukuta mbele ya timu ya taifa ya Burkina Faso ambayo ilitinga katika hatua ya fainali kwa ushindi wa mikwaju ya panati 4-2.

Timu hizo zilipigiana mikwaju ya panati baada ya kufungana bao moja kwa moja ndani ya muda wa dakika 120.

Kwa upande wa timu ya taifa uya Ivory Coast, yenyewe ilishindwa kufurukuta mbele ya wenyeji katika mchezo wa hatua ya nusu fainali uliopigwa jana katika uwanja wa Amahoro, baada ya kukubali kisago cha bao moja kwa sifuri.

Mchezo wa hatua ya fainali ya michuano hiyo utachezwa siku ya jumamosi kati ya wenyeji Rwanda dhidi ya timu ya taifa ya Burkina Faso.

No comments:

Post a Comment