KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Wednesday, January 12, 2011

Edin Dzeko ATUA RASMI CITY OF MANCHESTER.


Mshambuliaji mpya wa klabu ya Man City Edin Dzeko ameahidi kutoa ushirikiano wa kutosha ndani ya kikosi cha klabu hiyo ambacho msimu huu kimepania kumaliza katika nafasi nne za juu kwenye msimamo wa ligi kuu ya soka nchini Uingereza.

Edin Dzeko ametoa ahadi hiyo mjini Mamnchester alipokua akitambulishwa mbele ya waandishi wa habari baada ya kukamilisha taratibu zote za usajili wake akitokea kwenye klabu ya Wolfburg ya nchini Ujerumani kwa ada ya uhamisho wa paund million 27.

Amesema anatambua mazingira ya ligi ya nchini Uingereza ni mageni kwake lakini akaahidi kufanya jitihada za kuyazoea mazingira hayo kwa uharaka zaidi na kutimiza malengo yaliyowekwa.

Amesema anatambua kazi iliyo mbele yake ni ngumu hasa ukizingatia anatakiwa kukata kiu ya mashabiki wa Man city waliomsubiri kwa hamu kubwa, sambamba na kuziba nafasi iliyoachwa wazi na mshambuliaji wa kimataifa toka nchini Italia Super Mario Balotelli ambae ni majeruhi.

Nae meneja wa klabu ya Man City Roberto Mancini ambae aliongozana na Edwin Dzeko kwenye ukumbi wa mkutano na waandishi wa habari amesema amefurahishwa na ujio wa mshambuliaji huyo ambae anaamini atafanya makubwa kama ilivyokua nchini Ujerumani.

Mancini pia amezungumzia masikitiko ya kumkosa mshambuliaji Super Maerio Balotelli ambae kwa sasa anauguza jeraha la goti na imeshaelezwa itamchukua muda wa majuma manne yajayo kurejea tena uwanjani.

No comments:

Post a Comment