KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Wednesday, January 5, 2011

Edin Dzeko KUPIMWA AFYA LEO !!!


Mshambuliaji wa kimataifa toka nchini Bosnia Edin Dzeko hii leo alikua kwenye maandalizi ya safari ya kuelekea nchini Uingereza kwa ajili ya kufanyiwa vipimo vya afya yake kabla ya kukamilisha taratibu za usajili ndani ya klabu ya Man city.

Edin Dzeko aliripotiwa kuwa kwenye maandalizi hayo baada ya uongozi wa klabu ya Man City kukubali kiasi cha fedha kilichotakiwa na uongozi wa klabu ya Wolfburg kama ada ya uhsamisho wa mshambuliaji huyo ambae anatakiwa kwa udi na uvumba huko City Of Manchester.

Jana meneja wa klabu hiyo ya mjini Manchester Roberto Mancini, alithibitisha taarifa za uongozi wa ngazi za juu kukubali ombi hilo lakini akawataka waandishi wa habari kuwa watulivu hadi hapo dili la mchezaji huyo litakapo malizika kwa asilimia mia moja.

No comments:

Post a Comment