KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Wednesday, January 5, 2011

Hatem Ben Arfa AKAMILISHA MAKAZI ST JAMES PARK.


Winga wa kimataifa toka nchini Ufaransa Hatem Ben Arfa amekua mchezaji wa kwanza kusajiliwa na meneja wa sasa wa klabu ya Newcastle Utd Alan Pardew alitwaa madaraka hayo mara baada ya kutimuliwa kwazi kwa Criss Hughton mwishoni mwa mwaka jana.

Alan Pardew amekamilisha usajili wa winga huyo mwenye umri wa miaka 23, baada ya mkataba wa Hatem Ben Arfa kuitumikia The Magpies kwa mkopo kufikia kikomo mwezi huu.

Hatem Ben Arfa anasajiliwa moja kwa moja huko St James Park, huku akiwa na kumbu kumbu mbaya ya kukosa kipindi kirefu cha msimu huu, kufuatia kuumia mguu wake wa kulia ambao ulivunjika baada ya kuchezewa ovyo na kiungo wa klabu ya Man city Nigel De Jong.

Uongozi wa klabu yake ya zamani Olympic Marcell umemtakia kila la kheri mchezaji huyo ambae tayari ameshaitumikia Newcastle Utd michezo mitano huku akiwa bado hajafuinga bao hata moja.

No comments:

Post a Comment