KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Wednesday, January 5, 2011

LEO USHINDI LAZIMA !!!


Meneja wa klabu bingwa nchini Uingereza Chelsea, Carlo Ancelotti ameendelea kutoa kauli za kuonyesha kujiamini zaidi ndani ya klabu hiyo licha ya mwenendo wa matokeo ya kikosi chake kutokua mzuri.

Calro Aneceloti ameonyesha hali hiyo alipokua akijibu maswali ya waandishi wa habari ambao walimuuliza anatarajia nini kufuatia matokeo mabovu yanayomuandama katika kipindi hiki, ambapo amesema haofii lolote kwani bado yupo saaaana huko Stamford Bridge.

Ancelotti amesema haoni sababu ya kuhofia kibarua chake klabuni hapo ili hali bado anaonyesha uwezo mkubwa kupitia kikosi chake ambacho mwishoni mwa juma lililopita kilishindwa kuwika nyumbani mbele ya Aston Villa waliolazimisha sare ya mabao matatu kwa matatu.

Amesema mchezo wa hii leo watakaocheza ugenini huko Molineux ana matumaini ya kushinda na si kushindwa kama ilivyozoeleka kwa mashabiki wengi wanaokichukukia kikosi hake.

Hata hivyo mzee huyo wa kitaliano ametoa sababu za kujiamini huko ambapo amesema tayari kikosi chake kimesharejea katika hali nzuri ya kiushindani hasa ukizingatia katika michezo kadhaa iliyopita kimekua kikionyesha harakati za kusaka ushindi lakini makosam madogo madogo yamekua wakiwagharimu katika dakika za lala salama.

No comments:

Post a Comment