KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Wednesday, January 26, 2011

Edwin van der Sar AENDELEZA MSISITIZO WA KUTUNDIKA GLOVES.


Kipa wa kimataifa toka nchini Uholanzi na klabu ya Manchester United, Edwin van der Sar ameendelea kushikilia msimo wake wa kutundika gloves mwishoni mwa msimu huu.

Edwin van der Sar mwenye umri wa miaka 40 ametoa msimamo huo hii leo kupitia mtandao wa kampuni ya uwakala ambayo imekua ikifanya nae kazi katika kipindi chote cha maisha yake ya soka.

Katika taarifa hiyo iliyotolewa kwenye mtandao kampuni hiyo ya uwakala Edwin van der Sar ameeleza kuwa umewadia kwa yeye kupumzika licha ya kurejea msisitizo huo kila
mara, lakini hii leo amelazimika kufanya hivyo baada ya kujifikiria kwa muda mrefu.

Taarifa hiyo imeendelea kubainisha wazi kwamba viongozi pamoja na wachezaji wa klabu ya Man utd kila leo walikua wakimtaka abadili mawazo ya kutundika Gloves, lakini imemuuwia vigumu kuufuata ushauri wao hivyo ameona ni bora apumzike na kutoa nafasi kwa wachezaji wengine kama alivyofanya katika timu ya taifa ya Uholanzi mwaka 2008.

Kipa huyo aliesjiliwa na klabu ya Man utd mwaka 2005 akitokea Craven Cottege yalipo makao makuu ya klabu ya Fulham, pia ameleza sababu nyingine ya kutaka kufanya hivyo ni kutaka kupata muda wa kutulia na familia yake ambayo kwa kipindi kirefu imekua ikipata muda mchache wa kukaa nae.

Aidha sababu nyingine ni kupata wakati wa kumpa maliwazo mkewe kipenzi ambae matatizo ya kulemaa ugonjwa mbao aliupata Disemba 2009.

Kufautia maamuzi hayo ya Edwin van der Sar meneja wa klabu ya Man utd Sir Alexander Chapman "Alex" Ferguson amezungumza kwa majonzi kwa majonzi makubwa ambapo amesema hana jinsi ya kukubaliana na maamuzi ya kipa huyo aliedumu ndani ya himaya yake kwa kipindi cha miaka mitano iliyopita.

Amesema kipa huyo ni mtu safi na mara nyingi alimtumia kama mfano wa kuigwa ndani ya kikosi chake hivyo atamkumbukwa kwa umahiri na kujituma kwake anapokua mazoezini pamoja na kwenye michuano mbalimbali.

Maisha ya soka ya Edwin Van der Sar.

October 29-1970: Alizwaliwa Mjini Voorhout, Nchini Uholanzi.

1990: Alijiunga Na Klabu Ya Ajax Amsterdam.

1992: Alikuwa Miongoni Mwa Wachezaji Wa Ajax Waliotwaa Ubingwa Wa Kombe La UEFA.

1994: Alifanikiwa Kutwaa Ubingwa Wa Uholanzi Kwa Mara Ya Kwanza Akiwa Na Klabu Ya Ajax.

1995: Alikuwa Miongoni Mwa Wachezaji Wa Ajax Waliotwaa Ubingwa Wa Ligi Ya Mabingwa Barani Ulaya Na Akatangazwa Kuwa Kipa Bora Wa UEFA.

1998: Aliisaidia Timu Ya Taifa Ya Uholanzi Kufika Katika Hatua Ya Nusu Fainali Ya Kombe La Dunia Huko Nchini Ufaransa.

1999: Alijiunga Na Klabu Ya Juventus Akitokea Ajax, Na Kuwa Kipa Wa Kwanza Wa Kigeni Kucheza Ligi Ya Italia.

2000: Aliisaidia Timu Ya Taifa Ya Uholanzi Kufika Katika Hatua Ya Nusu Fainali Ya Michuano Ya Mataifa Ya Bara La Ulaya Iliyofanyika Nchini Uholanzi Pamoja Na Ubelgiji.

2001: Alijiunga Na Klabu Ya Fulham Ya Nchini Uingereza.

2005: Alijiunga Na Klabu Ya Manchester United Kwa Ada Ya Uhamisho Wa Paund Million 7.

2008: Aliisaidia Man Utd Kutwaa Ubingwa Wa Ligi Ya Mabingwa Barani Ulaya Baada Ya Kuokoa Penati Ya Nicolus Anelka.

2009: Aliweka Rekodi Ya Kucheza Dakika 1,311 Bila Kufungwa Bao Lolote Na Kujikuta Akikubali Kuruhusu Bao Katika Mchezo Wa Hatua Ya Fainali Ya Ligi Ya Mabingwa Barani Ulaya Dhidi Ya Fc Barcelona.

2010: Alitangaza Kustahafu Soka.

2011: Ameendelea na Msimamo Wake Wa Kustahafu Soka.


No comments:

Post a Comment