Meneja wa klabu ya Blackpool Ian Scott Holloway ameonyesha kukasirishwa na maamuzi ya muamuzi Peter Walton aliechezesha pambano la jana ambalo lilishuhudia kikosi chake kikizama nyumbani kufuatia kisago cha mabao matatu kwa mawili kilichotolewa na vinara wa ligi kuu ya soka nchini Uingereza Man Utd.
Ian Scott Holloway ameonyesha hali hiyo saa chache mara baada ya kipyenga cha mwisho kupulizwa huko Bloomfield Road ambapo amesema Peter Walton hakuutendea haki upande wa kikosi chake kwa maamuzi hafifu aliyoyatoa.
Amesema kikosi chake kilistahili kuzawadiwa mkwaju wa penati katika dakika za mwanzo za kipindi cha pili, baada ya beki wa kulia wa klabu ya Man utd Rafael Pereira da Silva kumsukuma kwa makusudi Luke Ivan Varney alipokua kwenye heka heka za kulishambulia lango na wapinzani hao.
Amesema hakuna ambae hakuona kitendo hicho na alisikitishwa na maamuzi ya Peter Walton pale alipoashiria mchezo uendelee ili hali kulikua hakuna haja ya kuamuru kitendo hicho.
Katika hatua nyingine meneja huyo wa klabu ya Blackpool amezungumzia hatua ya kupoteza mchezo huo wa jana ambapo amesema uzembe mkubwa uliofanywa na safu yake ya ulinzi uliwagharimu kiasi kikubwa hali ambayo imewafanya kupoteza point tatu muhimu nyumbani.
Amesema kiujumla safu yake ya ulinzi ilionyesha kutoyamudu mashambuzi ya Man Utd ambayo katika dakika 20 za mwisho za mchezo huo yalipamba moto hasa baada ya mshambuliaji wa kimataifa toka nchini Mexico Javier Hernández Balcázar Chicharito kuingia uwanjani huku akichukua nafasi ya mshambuliaji wa kimataifa toka nchini Uingereza Wayne Mark Rooney.
No comments:
Post a Comment