Mshambuliaji wa kimataifa toka nchini Senegal pamoja na klabu ya Blackburn Rovers, El-Hadji Diouf amembwatukia meneja wa klabu Queen Park Rangers Neil Warnock ambae amedai mchezaji huyo hakufanya kitendo cha uangwana kufuatia kauli aliyoitoa mara baada ya mchezo wa kombe la FA kumalizika mwishoni mwa juma lililopita.
Diouf ambae anatuhumiwa kusema maneno makali dhidi ya mshambuliaji wa klabu ya Queen Par Rangers Jamie Mackie mara baada ya kuvunjika mguu akiwa uwanjani katika mchezo huo wa kombe la FA, amesema hakuzungumza lolote kama inavyodaiwa na Warnock na ameshangazwa na hatua ya kuhusishwa na kutoa maneno hayo makali.
Amesema mbali na kutokuzungumza lolote akiwa uwanjani pia hakuzungumza lolote mara baada ya mchezo huo kumalizika kwenye uwanja wa Ewood Park, ambapo wenyeji walifanikiwa kupata ushindi wa bao moja kwa sifuri.
Kubwa linalodaiwa na meneja wa klabu ya Queen park Rangers, Neil Warnock ni kwamba El-Hadji Diouf alidai Jamie Mackie hakua mkweli na dhamira yake alitaka kumshawishi muamuzi ili afahamu amevunjwa mguu Gael Givet wa Bluckburhn Rovers ili aonyeshwe kadi nyekundu.
Hata hivyo Diouf amemtakia kila la kheri Jamie Mackie katika kipindi hiki kugumu cha kuuguza jeraha la mguu wake na bado akaendelea kusisitiza kwamba kwa sasa anajitahidi kushughulika na tabia yake ambayo siku za nyuma ilimuweka pabaya.
Mbali na kuvieleza vyombo vya habari Nail Warnock alidiriki kumuita mchezaji huyo wa zamani wa klabu ya Liverpool pamoja na Bolton Wanderers panya anaeng’ata na kupuliza kufuatia vitendo vyake viovu anavyovifanya akiwa uwanjani.
Nail Warnock pia alimtaka Diouf kutambua kwamba wakati huu, uliopo sasa si wakutoleana maneno machafu bali ni wakati wa kucheza soka kwa mchezaji yoyote alietakasika.
No comments:
Post a Comment