KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Friday, January 14, 2011

Shaun Wright-Phillips AWANIWA VIKALI NA FULHAM.


Siku moja baada ya kuthibitishwa uwepo wa safari ya kuondoka kwa winga wa kimataifa toka nchini Uingereza na klabu ya Man city Shaun Wright-Phillips, maneja wa klabu ya Fulham Mark Hughes amesema kuna uwezekano mkubwa kwa mshambuliaji huyo kuelekea Craven Cottege.

Mark Hughes ametoa tambo hizo alipozungumza na waandishi wa habari ambapo amesema tayari uongozi umeshampa nafasi ya kufanya usajili kwa mchezaji anaeona anamfaa katika kipindi hiki kwa malengo ya kuboresha kikosi chake ambacho kimerejea kwenye harakati za ushindani.

Amesema ushirikiano mzuri kati yake na viongozi wa klabu hiyo ndio unafanikisha safari ya winga huyo kurejea jijini London ambapo kwa mara ya mwisho alikuawepo jijini humo akiitumikia klabu ya Chelsea ambayo ilimsajilia kitokea Man city mwaka 2005.

Hata hivyo Fulham bado wapo kwenye changamoto nzito ya kumsajili winga huyo mwenye umri wa miaka 29 kufuatia klabu za West Ham utd pamoja na Birmingham City kuonyesha nia ya kutaka kumsajili.

No comments:

Post a Comment