KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Thursday, January 13, 2011

Mauro Boselli KUONDOKA WIGAN.


Mshambuliaji wa kiamataifa toka nchini Argentina na klabu ya Wigan Mauro Boselli kwa sasa anajiandaa kujiunga kwa mkopo na klabu ya Genoa ya nchini Hispania.

Meneja wa klabu ya Wigan Roberto Martinez amesema mshambuliaji huyo aliesajiliwa huko DW Stadium kwa ada ya uhamisho wa paund million 6.5 akitokea nyumbani kwao kwenye klabu ya Estudiantes ameshinikiza kuondoka klabuni hapo kwa lengo la kupata changamoto mpya mbali na anazozipata sasa kwenye ligi kuu ya soka nchini Uingereza.

Kama hiyo haitoshi bado Mauro Boselli alithibitisha kuwepo kwa safari hiyo ya nchini Hispania kwa kuandika ujumbe kwenye ukurasa wake wa mtandao wa Twitter, ambao unasomeka “Nitakua na furaha zaidi endapo nitajiunga na klabu ya Genoa kwa muda wa miezi sita iliyosalia msimu huu”.

No comments:

Post a Comment