KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Wednesday, January 19, 2011

Eric Daniel Pierre Cantona ATANGAZWA KUWA BOSI.


Gwiji wa soka toka nchini Ufaransa mbae alimalizeia soka lake kwenye klabu ya Man utd ya nchini Uingereza Eric Daniel Pierre Cantona ameteuliwa kuwa mkurugenzi wa soka wa klabu ya New York Cosmos ya nchini Marekani.

Eric Cantona ameteuliwa kushika wadhifa huo, baada ya kuzinduliwa kwa mradi wa soka na sanaa ndani ya klabu hiyo ambapo hatua hiyo imefanikishwa na makamu mwenyekiti wa zamani wa klabu ya Tottenham Hotspurs Paul Kemsley.

Cantona mwenye umri wa miaka 44, amesema kwake imekua faraja kubwa kuteuliwa kushika wadhifa huo na ameahidi kufanya kazi kwa ushirikiano mkubwa na viongozi wenzake kwa minajili ya kuifikisha mbali klabu hiyo ya nchini Marekani.

No comments:

Post a Comment