KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Wednesday, January 19, 2011

Leeds United v Arsenal - FA Cup 3rd Round Replay.


Jeshi la Ashburton Grove Arsenal muda mchache ujao litakua na kibarua kingine cha kuhakikisha linavuka kwenye hatua ya tatu ya michuano ya kombe la chama cha soka nchini Uingereza FA, pale litakapokaribishwa huko Eland Road na wenyeji wao Leeds Utd.

Jeshi hilo lenye maskani yake makuu kaskazini mwa jiji la London limelazimika kuifunga safari hadi mjini Leeds kufuatia kushindwa kuwika nyumbani katika mchezo wa kwanza wa hatua ya tatu ya michuano hiyo uliochezwa kwenye uwanja wa Emirates majuma mawili yaliyopita ambapo wenyeji Arsenal walilazimisha sare ya bao moja kwa moja.

Wenyeji wa mchezo huo wa leo Leeds Utd watamkosa mshambuliaji wao Luciano Becchio anaenongoza kwa upachikaji wa mabao klabuni hapo, baada ya kuumia mgongo mwishoni mwa juma lililopita kwenye mchezo wa ligi dhidi ya Scunthorpe huku beki aliejiunga na klabu hiyo kwa mkopo akitokea West ham utd George McCartney akiwa matatizoni kufuatia mkataba wake kumalizika na sasa unajadiliwa upya hivyo hatocheza na nafasi yake itachukuliwa na Ben Parker.

Meneja wa klabu ya Leeds Utd Simon Grayson amesema katika mchezo wa hii leo wapinzani wao watakua na jukumu zito la kuhakikisha wanazuia aibu inayowanyelea baada ya kushindwa kuwika nyumbani kwao Emirates majuma mawili yaliyopita kufuatia kikosi chake kuonyesha kandanda safi.

Kwa upande wa Arsenal wanakwenda uwanjani hii leo bila ya kuwa na kipa wao tegemezi Lucas Fabianski, kiungo Abou Diaby pamoja na beki Sebastian Squilaci huku Bacary Sagna akitarajiwa kujumuishwa kikosini baada ya kumaliza adhabu ya kutokucheza michezo mitatu mfululizo kufuatia kadi nyekundu aliyoonyeshwa kwenye mchezo wa ligi dhidi ya Man City.


Meneja wa klabu ya Arsenal Arsene Wenger tayari ameshawaeleza wachezaji wake kwamba itawalazimu kucheza kufa na kupona usiku huu, ili waendelee kuwepo kwenye michuano hiyo ya kombe la FA ambayo kwa mara ya mwisho ilishuhudia wakiibuka vinara mwaka 2005.

Amesema msululu wa majeruhu unaomuandama kwa sasa bado utaendelea kumuandama na anafikiria huenda wachezaji walio kwenye msululu huo wakaanza kurejea tena uwanjani baada ya majuma mawili yajayo wakitaguliwa na Abou Diaby.

No comments:

Post a Comment