Kipa wa timu ya taifa ya Ghana Black Stars Richard Paul Franck Kingson amesema kuna ulazima mkubwa wa kiungo wa klabu ya Chelsea Michael Kojo Essien kuitwa kwenye kikosi cha timu ya taifa baada ya kukosekana kwenye timu hiyo kwa kipindi kirefu kilichopita.
Richard Paul Franck Kingson anaeitumikia klabu ya Blackpool ya nchini Uingereza ametoa kauli hiyo, huku timu ya taifa ya Ghana ikitarajia kuingia kambini siku za hivi karibuni kujiandaa na mchezo wa kimataifa wa kirafiki utakaochezwa mwanzoni mwa mwezi ujao.
Amesema uwepo wa kiungo huyo mwenye umri wa miaka 28 kutanyanyua ari ya wachezaji wengine ndani ya timu hiyo ambayo kwa mara mwisho ililazimishwa matokeo ya sare na timu ya taifa ya Sudan kwenye mchezo wa kuwania nafasi ya kufuzu kucheza fainali za mataifa ya bara la Afrika mwaka 2012.
Amesema mbali na kuhitajika kwa kiungo huyo, pia usaidizi wake katika nafasi ya kiungo unahitajika kwa hali na mali hivyo anaamini kocha mpya wa timu ya taifa ya Ghana Goran "Plavi" Stevanović atamjumuisha kwenye kiksoi chake atakachokiita mwanzoni mwa juma lijalo.
Michael Essien hajawahi kuitwa kwenye timu ya taifa ya Ghana toka alipopata jeraha la goti kwenye fainali za mataifa ya bara la Afrika zilizofanyika nchini Angola mwanzoni mwa mwaka jana ambapo kiungo huyo aliumia katika mchezo wa kwanza wa kundi la nne dhidi ya timu ya taifa ya ivory Coast.
Mbali na kukabiliwa na mchezo wa kimataifa wa kirafiki mwanzopni mwa mwezi ujao pia timu ya taifa ya Ghana inabiliwa na michezo ya kundi la 9 ya kuwania nafasi ya kucheza fainali za mataifa ya bara la Afrika na mpaka sasa timu hiyo imeshashuka dimbani mara mbili.
No comments:
Post a Comment